Kituo cha habari cha Mas’haf al Madina kimezinduliwa na Jumuiya ya Uchapishaji na Usambazaji wa Qur’ani Tukufu ya Mfalme Fahad mjini Madina, Saudi Arabia kwa lengo la kutoa huduma za intaneti katika nyanja za Qur’ani na sayansi za kitabu hicho.
Gazeti la al Riyadh limeandika kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Uchapishaji na Usambazaji Qur’ani ya Mfalme Fahad, Muhammad Salim bin Shadid al Aufi amesema kituo hicho cha intaneti kimepewa anwani ya: mushaf-services.qurancomplex.gov.sa.
Kituo hicho pia kina maelezo kamili kuhusu nakala ya Qur’ani iliyoandikwa kwa hati za Kiothmani.
Pamoja na mambo mengine kituo hicho kina tafsiri za Qur’ani, misamiati migumu ya Qur’ani, irabu ya aya za kitabu hicho, sababu za kuteremshwa sura na aya za Qur’ani na kiraa ya Qur’ani ya wasomaji mashuhuri. 813221