Mashindano hayo yatafanyika katika mji mkuu wa Qatar Doha.
Awamu hii ya mwisho ya mashindano hayo itafunguliwa na Waziri wa Wakfu wa Qatar Ghaith bin Mubarak na kuonyeshwa moja kwa moja katika televisheni ya watoto ya al Jazeera.
Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zitashirikisha kamati ya majaji wa kimataifa wa Qur’ani na kiraa ya wasomaji watatu mashuhuri wa Qur’ani duniani.
Awamu hii ya mwisho ya kiraa ya Qur’ani ya watoto ya kanali ya televisheni ya al Jazeera itawachuanisha watoto 63 kutoka mabara matano ya dunia.
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar imetenga zawadi tano za fedha taslimu kwa washindi wa mashindano hayo yatakayosimamiwa na majaji na wataalamu mashuhuri wa sayansi ya Qur’ani kutoka nchi mbalimbali duniani. 813373