IQNA

Warsha ya Mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu kufanyika Iran

15:35 - June 23, 2011
Habari ID: 2143146
Mji mtakatifu wa Qum nchini Iran utakuwa mwenyeji wa warsha ya kuhusu mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu.
Shariyar Shojaeepur Mkurugenzi wa Taasisi ya Utamaduni na Utafiti wa Kiislamu amesema warsha hiyo itaanza Juni 23-25.
Amesema katika warsha hiyo wasomi mashuhuri wa Iran watawasilisha makala kuhusu mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu. Aidha wataalamu wa kiuchumi kutoka Chuo Kikuu cha Teknologi Mara cha Malaysia watashiriki katika kikao hicho.
Warshi hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Utamaduni na Utafiti wa Kiislamu na inalenga kuleta pamoja uzoefu wa wataalamu wa uchumi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Malaysia katika uga wa mfumo wa uchumi wa Kiislamu. Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa kitashirikiana katika kuandaa warsha hiyo.
813464
captcha