Kwa mujibu wa gazeti la Al-Yawm As-Sabi, Sheikh Shoaisha ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Makarii na Mahafidh wa Qur'ani nchini Misri aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 89.
Ustadh Shoaisha alizaliwa Kafarsheikh kaskazini mwa Misri mwaka 1343 Hijri (1922). Alianza kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu akiwa mtoto mdogo. Shoaisha alipata umashuhuri kama karii kuanzia mwaka 1936 alipokuwa akihudhuria darsa za kiraa ya Qur'ani mjini Mansura. Alianza kusoma Qur'ani katika Radio ya Misri mwaka 1939. Shoaisha aliathiriwa sana Ustadh Sheikh Muhammad Raf'at, karii mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu. Awali alifuata mbinu ya usomaji wa Raf'at lakini baadaya aliibua mbinu yake ya kipekee ya kiraa.
Ustadh Shoaisha alitembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mara kadhaa kama jaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.
Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa IQNA lenye makao yake Iran linatoa salamu zake za rambi rambi kufuatia kifo cha karii na msomaji huyo maarufu wa Qur'ani Tukufu.
IQNA ilichapisha makala maalumu kuhusu Ustadh Shoaisha miaka mitatu iliyopita ambayo inaweza kupatikana katika
http://www.iqna.ir/Rayehe/47/Main.php
814158