IQNA

Ahmadinejad: Ugaidi, dawa za kulevya hatari kubwa kwa mwanadamu

14:08 - June 26, 2011
Habari ID: 2144448
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametaja ugaidi na dawa za kulevya kuwa hatari kubwa kwa jamii ya mwanadamu.
Rais Ahmadinejad ameyasema hayo mjini Tehran alipokutana na Rashid Meredov Waziri wa Mambo ya Nje wa Turkmenistan.
Kwingineko, Rais Ahmadinejad amesema mazungumzo ndio njia bora ya kutatua matatizo ya kieneo. Ameyasema hayo katika mkutano wake na Yusuf Bin Alawi Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman. Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa madola ya Kimagharibi si marafiki wa kweli wa nchi za eneo la Mashariki ya Kati.
815157
captcha