Kituo cha habari cha Lebanonfiles kimeripoti kuwa shughuli hiyo itasimamiwa na kamati ya kukumbuka mwaka wa kwanza tangu kufariki dunia Allamah Fadhlullah. Kamati hiyo inajumuisha wananchi wa Lebanon na wapenzi wa mwanazuini huyo wa Kiislamu.
Allamah Muhammad Hussein Fadhlullah alifariki dunia tarehe 4 Julai mwaka 2010 akiwa na umri wa miaka 75. Mwanazuoni huyo ameandika tafsiri ya "Min Wahyil Qur'ani" yenye juzuu 25 inayotoa mafunzo ya kimalezi, kisayansi na kadhalika. Mbinu ya tafsiri ya Allamah Fadhlullah inatajwa kuwa inashabihiana na ile ya marehemu Sayyid Qutb katika kitabu cha "Fi Dhilal al Qur'ani". 815350