IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu zimeongezeka baada ya kuchaguliwa Obama

11:00 - June 27, 2011
Habari ID: 2145034
Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu kuhusu chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu kote Marekani umeonyesha kuwa asilimia 45 ya Wamarekani wanaamini kuwa Uislamu unakinzana na thamani za Kimarekani.
Baraza hilo linasema utafiti huo unaonyesha kuwa chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) nchini Marekani imeongezeka baada ya kuchaguliwa rais Barack Obama. Makundi ya mrengo wa kulia ya chama cha Republican yamekuwa yakieneza hisia za chuki dhidi ya Waislamu na kudai kuwa sheria za Kiislamu zitatelekezwa nchini humo.
Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu lenyewe limelengwa katika chuki hizo na kudaiwa kuwa linaunga mkono ugaidi. Baraza hilo limetajwa pamoja na mashirika mengine 250 kuwa yanaunga mkono Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas.
815467
captcha