IQNA

Waliolipua Haram ya Maimam Samurra wahukumiwa kifo

0:57 - June 29, 2011
Habari ID: 2146158
Watu waliolipua Haram ya Maimam Hadi na Askari (as) katika mji wa Samurra nchini Iraq wamehukumiwa kifo leo sambamba na shughuli ya kukumbuka siku ya kuuawa shahidi Imam Mussa al Kadim (as).
Maafisa wa Haram ya Imam Kadhim (as) wametangaza habari hiyo leo wakati wa shughuli za maombolezo ya kukumbuka siku ya kuuawa shahidi mtukufu huyo.
Habari hiyo imetangazwa wakati Waislamu walipokuwa katika maombolezo na majlisi za kukumbuka mashaka yaliyompata mjukuu huyo wa Mtume Muhammad (saw).
Shughuli ya maombolezo hayo imewashirikisha watu milioni nne waliokwenda kuzuru kaburi la Imam Kadhim (as) kwa amani kamili na hadi tunaandika habai hii Waislamu walikuwa bado wanamiminika katika haramu huyo tukufu.
Haram ya Maimam Hadi na Askari (as) ilishambuliwa na magaidi kwa milipuko ya mabomu tarehe 22 Februari mwaka 2006 na sehemu moja ya minara yake iliharibiwa katika shambulizi hilo.
Miaka miwili iliyopita polisi ya Iraq ilimtia nguvuni Abdul Samad al Bazi aliyetekeza shambulizi hilo la kigaidi akijaribu kuingia nchini humo na kumpeleka Baghdad kwa uchunguzi zaidi. 816965

captcha