IQNA

Mji wa Qur’ani wapangwa Iraq

14:33 - June 29, 2011
Habari ID: 2146502
Idara ya Gavana wa mkoa wa Basra nchini Iraq imetangaza mpango wa kuanzisha ‘Mji wa Qur’ani’ katika eneo la kusini mwa nchi hiyo kwa ushirikiano na Kituo cha Darul Qur’an al Karim kinachofungamana na Taasisi ya Haram ya Imam Husseini AS.
‘Mji wa Qur’ani’ mkoani Basra utajumuisha shule ya chekechea, chuo cha Qur’ani na chuo kikuu cha Qur’ani maalumu kwa ajili ya kuhifadhi Qur’ani na mafunzo ya sayansi za Qur’ani.
Abdul Karim al Rumi mkuu wa masuala ya sanaa katika idara ya gavana wa Basra amesisitiza umuhimu wa Darul Qur’an Karim katika kutoa mafunzo ya sayansi za Qur’ani.
816049
captcha