IQNA

OIC yabadilisha jina na nembo yake

14:39 - June 29, 2011
Habari ID: 2146556
Jina la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (Organization of the Islamic Conference) ambalo limekuwa likitumika tangu miaka 42 iliyopita lilibadilishwa Juni 28 mjini Astana Kazakhstan na kuwa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (Organization of the Islamic Cooperation) ili kwenda sambamba na majukumu yake.
Katika sherehe zilizodhudhuriwa na Rais Nursultan Nazarbayev Rais wa Jamhuri ya Kazakhstan na Katibu Mkuu wa OIC Prof. Ekmeledin Ihsanoglu, nchi zote wananchama zilishuhudia kubadilishwa jina na nembo ya OIC. Utambulisho mpya wa OIC unaashiria kubadilisha utendaji kazi wa jumuiya hii inayozikutanisha pamoja nchi za Kiislamu duniani. OIC sasa inalenga kuboresha utendaji kazi wake kama taasisi yenye ushawishi katika uga wa kimataifa hasa katika sekta za uchumi, siasa, utamaduni na jamii.
Rais wa Kazakhstan amesema kuwa Waislamu wanadhibiti asilimia 70 ya akiba ya maliasili duniani lakini wanamiliki tu asilimia 7 ya biashara ya dunia. Kwa kuzingatia hilo amesema kuna haja ya fikra mpya za kiuchumi ili kuleta maendeleo katika ulimwengu wa Kiislamu.
Naye Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa utambulisho na hati ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu haijabadilishwa licha ya kubadilishwa jina lake na kuwa Jumuiya ya Ushirkiano wa Kiislamu.
Ali Akbar Salehi ambaye anashiriki mkutano wa OIC mjini Astanan, Kazakhstan amesema kuwa jina jipya la jumuiya ya OIC linaoana na kazi za taasisi hiyo ya kimataifa. Amezungumzia pia uwezo mkubwa wa kiuchumi wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC na kusema JKI ni nchi iliyopiga hatua kubwa katika masuala ya viwanda na uchumi na inaweza kutoa msaada kwa nchi nyingine za Kiislamu.
817342
captcha