Waziri Mkuu wa Malaysia amesema katika barua hiyo kwamba lengo la msafara huo ni kufikisha misaada ya kibinadamu kwa raia wa Gaza na ameutaka Umoja wa Mataifa kuwalinda watu walioko kwenye msafara huo.
Najib Tun Razak ameutaka umoja huo kuwatuma wawakilishi wake kwenda kuchunguza bidhaa zinazobebwa na meli za msafara huo na kuwahakikishia walimwegu na utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba meli hizo zinabeba misaada ya kibinadamu.
Waziri Mkuu wa Malaysia ameongeza kuwa wanaharakati wa haki za binadamu wa Malaysia wamo katika msafara huo unaojumuisha wawakilishi wa nchi mbalimbali duniani.
Vilevile amemtaka Ban Ki-moon autahadharishe utawala ghasibu wa Israel juu ya hatari za kutumia mabavu dhidi ya meli za msafara wa Uhuru-2. 817384