IQNA

Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani yaanza Tehran

11:26 - June 30, 2011
Habari ID: 2146841
Mashindano ya Kimataifa ya 28 ya Qur’ani Tukufu yameanza mjini Tehran katika sherehe iliyohudhuriwa na Rais Mahmoud Ahmadinejad, viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa Iran na wageni waalikwa kutoka nchi mbalimbali duniani.
Sherehe hizo zilianza kwa wimbi wa taifa na kufuatiwa na kisomo cha Qur’ani Tukufu. Baadaye kidogo Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano ambako ndiko mashindano hayo yanakofanyika, ulitumbuizwa kwa kadisa na nyimbo za kumisifu Mtume (saw) na Maimamu watoharifu katika kizazi chake.
Mkuu wa Shirika la Wakfu na Hija la Iran Hujjatul Islam Walmuslimin Ali Muhammad alianza kuhutubia hadhara hiyo kwa kutoa ripoti kuhusu mashindano ya 28 ya Qur’ani Tukufu ya Tehran akisema kuwa wawakilishi wa nchi 61 wanachuana katika mashindano ya sasa ikiwa ni pamoja na mahafidhi wa Qur’ani 43 na makarii 53.
Hujjatul Islam Ali Muhammadi amesema mashindano ya Qur’ani yanayofanyika katika nchi zote za Kiislamu isipokuwa Libya na Malaysia huwa na kitengo kimoja tu cha hifdhi ya Qur’ani lakini nchini Iran mashindano hayo hujuisha kiraa na hifdhi. Ameongeza kwamba mashindano hayo pia yanajumuisha uandishi wa makala kuhusu sababu za kubakia nyuma Waislamu, mwamko wa Kiislamu katika mtazamo wa Qur’ani, kazi katika mtazamo wa Qur’ani, njia za kutambua fitina katika Qur’ani na kuanisika na Qur’ani.
Msomaji mashuhuri wa Misri Abdulfattah Tarouti aliburudisha nyoyo za washiriki katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo kwa kusoma baadhi ya aya za kitabu cha Mwenyezi Mungu.
Baada ya ufunguzi wa mashindano hayo, Rais Mahmoud Ahmadinejad amehutubia hadhirina akiitaja Qur’ani kuwa ni kitabu kinachomwondoa mwanadamu katika giza na kumwonyesha njia iliyonyooka. 817755
captcha