IQNA

Mufti wa Misri aidhinisha sherehe za tarehe 15 Sha’aban

16:52 - July 02, 2011
Habari ID: 2147187
Mufti wa Misri ametoa fatuwa ya kuidhinisha kufanyika sherehe za siku ya kuadhmisha kuzaliwa Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake) tarehe 15 ya mwezi wa Sha’aban.
Kwa mujibu wa tovuti ya Noon, Sheikh Ali Gomaa amesema kuwa, ‘Hafla na sherehe za kidini katika misikiti na vituo vya kidini hutofautiana. Nchini Misri inaruhusiwa kuandaa sherehe kwa mnasaba wa sikukuu ya kuzaliwa Imamu wa 12 wa Waislamu wa madhehebu ya Shia’.
Mufti wa Misri aliwahi kutoa fatuwa ya kuruhusu kutembelea au kufanya ziara katika makaburi na kusema kuwa ziara hizo si ishara ya kufri au shirki.
Tarehe 15 Sha'abani ndiyo siku aliyozaliwa ndani yake Imam Mahdi (as) Imam wa 12 katika kizazi cha Mtume Muhammad (saw) ambaye anasubiriwa na walimwengu kuja kuijaza dunia uadilifu na usawa baada ya kujazwa dhulma na uonevu. Imam Mahdi (as) yuko ghaibu kwa amri ya Mola Muumba na atadhihiri katika akheri zamani kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (SW).
Chini ya utawala wa dikteta Hosni Mubarak aliyetimuliwa madarakani Misri, Waislamu Mashia nchini humo hawakuruhusiwa kuandaa hafla za kidini au kujenga misikiti.
817704
captcha