IQNA

Maonyesho ya Hisa ya Waislamu katika Uwanja wa Sayansi na Teknolojia kufanyika California

20:24 - July 02, 2011
Habari ID: 2147692
Maonyesho ya mchango wa Waislamu katika Uwanja wa Sayansi na Teknolojia yatafanyika tarehe 3 Septemba mwaka huu katika jimbo la California Marekani.
Shirika la habari la Imarati limeripoti kuwa maonyesho hayo yatasimamiwa na taasisi ya MTI Stiudios (taasisi ya ushauri na utaalamu wa sanaa za usanifu majengo) yenye makao Dubai na Cape Town Afrika Kusini.
Maonyesho hayo yatafanyika katika jumba la makumbusho la The Tech Museum la California ambalo ni miongoni mwa majumba mashuhuri ya makumbusho ya masuala ya teknolojia.
Maonyesho hayo yataonyesha kazi za wasomi na maulamaa wa Kiislamu katika nyanja za sayansi na teknolojia katika vipindi tofauti vya historia.
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya MTI Studios amesema makundi ya wataalamu yatakagua pia maonyesho hayo.
Maonyesho hayo tayari yamekwishafanyika katika jimbo la New Jersey na kuwavutia watu wengi. 818539

captcha