Akizungumza na IQNA, Hujjatul Islam Alireza Shasavani amesema kozi hiyo itawahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu vya sayansi za Qur’ani na mafundisho ya Kiislamu.
Amesema wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza watahifadhi juzuu kadhaa katika msimu wa majira ya joto na hatimaye katika kipindi chote cha mwaka wanatazamiwa kuhifadhi Qur’ani nzima.
Amesema washiriki watahifadhi kurasa mbili za Qur’ani kila siku na watahudhuria darsa za tafsiri kabla ya kuhifadhi.
818439