IQNA

Qur'ani Tukufu ni Katiba ya umma wa Kiislamu

17:23 - July 04, 2011
Habari ID: 2148811
Karii Mpalestina anayeshiriki katika Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran amesema kuwa Qur'ani Tukufu ni katiba ya umma wa Kiislamu kote duniani na amewataka Waislamu wajitahidi kukifahamu kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na kutekeleza maamrisho yake.
Ayub Yusuf Musa raia wa Palestina mwenye umri wa miaka 23 amesema katika mahojiano na IQNA kuwa, 'Qur'ani Tukufu ni chanzo cha umoja na ustawi wa Waislamu na mataifa ya Waislamu'.
Kuhusu mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran mwaka huu amesema: "Hii ni mara ya pili nakuja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Nilishiriki katika mashindano ya 25 ya kimataifa ya Qur'ani yaliyofanyika Mash'had'.
Amesema kiwango cha mashindano ni kizuri sana na kinahisika hata kabla ya majaji kutangaza matokeo yao

819839
captcha