IQNA

Mashindano ya Qur'ani ni ishara ya kuzingatiwa Uislamu nchini Iran

17:37 - July 04, 2011
Habari ID: 2148819
Kaundaliwa mashindano ya kimaaifa ya Qur'ani kila mwaka nchini Iran ni ishara kuwa nchi hii inazingatia kuenezwa Uislamu duniani.
Hayo ni kwa mujibu Shuaib Chub karii anayewakilsha Senegal katika Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran yanayofanyika kati ya 27 na 2 Shaaban. Katika mahojiano na IQNA, amesema kuandaliwa mashindano ya Qur'ani kuna uhusiano wa moja kwa moja na mikakati ya Iran ya kueneza Uislamu duniani na kuleta umoja wa Kiislamu. Ameongeza kuwa mashindano ya Qur'ani yanayofanyika Iran ni fursa ya Waislamu kutoka maeneo yote duniani kujuana na kubadilishana mawazo. Karii huyu wa Senegal amesema kiwango cha mashindano ya Qur'ani ya Iran ni cha juu sana ikiliganishwa na mashindano yanayofanyika katika nchi zingine.
819591
captcha