IQNA

Vijana wana nafasi muhimu katika mwamko wa Kiislamu

17:31 - July 04, 2011
Habari ID: 2148822
Waziri wa Usalama wa Iran amesema kuwa vijana wana nafasi muhimu katika mwamko wa Kiislamu ambao umekita mizizi katika nchi za Kiislamu.
Sheikh Heidar Muslehi ameyasema hayo Julai tatu usiku katika hotuba aliyoitoa katika Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran.
Ameongeza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kigezo kwa harakati za mwamko wa Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu.
Ameongeza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameleta mwamko miongoni mwa vijana Waislamu duniani.
Sheikh Muslehi amesema kuwa kushiriki nchi 60 katika Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran ni mafanikio makubwa kwa Iran. Aidha amesifu kiwango cha mashindano hayo ya Qur'ani na kusema kuwa yatakuwa na nafasi muhimu katika kustawisha Qur'ani Tukufu na utamaduni wa Qur'ani nchini Iran.
819744
captcha