Kwa mujibu wa tovuti ya Gaboneco, kongamano hilo linafanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya Uchumi na Idara ya Kibiashara ya Gabon.
Lengo la kongamano hilo limetajwa kuwa ni kuchunguza uwezo wa Gabon katika kuanzisha benki za Kiislamu, kutumia suhula za kifedha kwa mujibu wa sheria za Kiislamu na kuanzisha mfumo wa kifedha wa Kiislamu ili kuwavutia wawekezaji Waislamu na wasiokuwa Waislamu katika sekta ya kifedha ya Kiislamu.
Aidha kutakuwa na warsha itakayoendeshwa na wawakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Kiislamu kuhusu nafasi ya mfumo wa kifedha wa Kiislamu katika kuimarisha miundombinu ya kiuchumi ya Gabon.
820355