Kituo cha habari cha Dubaijamaat kimeripoti kuwa semina hiyo itafanyika kwa hima ya Kamati ya Ulinganiaji ya kituo cha Shia Ithnaashari mjini Dubai katika ukumbi wa Hathrat Abbas (as).
Semina hiyo ya siku mbili itafanyika kwa mnasaba wa kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni mwezi Qur'ani ilioteremshwa ndani yake kwa lengo la kutayarisha uwanja mzuri wa kuielewa Qur'ani Tukufu kama hatua ya kwanza ya kustafidi na hazina inayotoa uhai ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Miongoni mwa maudhui zitakazojadiliwa katika semina hiyo ni pamoja na Qur'ani na hakika ya kitabu hicho cha mbinguni, chanzo na asili ya Qur'ani Tukufu, lengo la udharura wa kuteremshwa Qur'ani, sababu za kuteremshwa Qur'ani, ujumbe wa Qur'ani, walengwa wa Qur'ani, mashukio ya mwisho ya walioamini Qur'ani, daraja za ujumbe wa Qur'ani na kadhalika. 823948