IQNA

Bunge la Palestina lataka OIC iunge mkono taifa la Palestina

9:19 - July 14, 2011
Habari ID: 2154232
Naibu Spika wa Bunge la Palestina Ahmad Bahar ametoa wito kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu kupeleka kadhia ya Palestina na vikao vya kimataifa.
Katika mazungumzo ya simu, Bahar amemfahamisha Ihsanoglu kuhusu mateso wanayofanyiwa wafungwa wa Kipalestina katika jela za kuogofya za utawala haramu wa Israel. Aidha wamejadili ukandamizaji wa Wapalestina unaofanya na utawala wa Kizayuni huko Quds.
Aidha Bahar amesema kuna haja OIC kuchukua hatua imara zaidi kuwatetea Wapalestina. Afisa hiyo wa Palestina pia amemtaka Katibu Mkuu wa OIC atembelee Ukanda wa Ghaza ili hiyo iwe hatua ya kwanza ya kivitendo ya kuvunja mzingiro wa utawala haramu wa Israel huko Ghaza. Katibu Mkuu wa OIC ameadhidi kuchunguza uwezekano wakutembelea Ghaza.
825582
captcha