IQNA

Msikiti wa Strasburg kufunguliwa mwezi wa Ramadhani

13:08 - July 16, 2011
Habari ID: 2155139
Viongozi wa Waislamu huko Strasburg Ufaransa wametangaza kuwa msikiti wa jamia utafunguliwa katika eneo la Heyrits katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mkurugenzi wa ujenzi wa msikiti huo Foad Doai amesema ujenzi wa msikiti huo bado unaendelea na kufuatia idhini ya kamati ya usimamizi, msikiti huo utatumika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Amesema kamati ya usimamizi imekagua awamu ya kwanza ya ujenzi wa msikiti huo na kuongeza kuwa awamu ya pili bado haijakaguliwa.
Ameongeza kuwa Sala ya Idul Fitr itasaliwa katika msikiti huo na baada ya hapo kufungwa kwa muda wa miezi miwili ili ujenzi ukamilike.
826136
captcha