Kituo cha Taibanews.com kimeripoti kuwa mashindano hayo yaliyoanza tarehe 5 Rajab katika msikiti wa Mtume mjini Madina yataendelea hadi tarehe 27 Shaaban.
Mashindano hayo yanafanyika katika vitengo saba vya hifdhi na kiraa katika anga ya kiroho ndani ya Masjidunnabi (saw).
Lengo la kufanyika mashindano hayo ni kutayarisha uwanja mzuri kwa vijana kwa ajili ya kuhifadhi Qur'ani katika kipindi kifupi na kutumia vyema kipindi cha mapumziko ya kiangazi.
Washindi watapewa stashahada ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu. 826186