Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Quds Tukufu Sheikh Ikrima Sabri ametoa taarifa akilaani hatua ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) la kuuarifisha mji mtakatifu wa Quds kuwa ni mji mkuu wa wa utawala ghasibu wa Israel.
Taarifa hiyo imesema: "Uamuzi wa UNESCO wa kuutangaza mji unaokaliwa kwa mabavu wa Baitul Muqaddas kuwa ni mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israel ni ishara kwamba jumuiya hiyo ya kimataifa imekiuka majukumu yake ya kisheria."
Sheikh Sabri amesema uamuzi kama huo uko nje ya majukumu na kazi za UNESCO na iwapo jumuiya hiyo itathibitisha habari hilo basi huo utakuwa uamuzi usiokuwa wa kuwajibika na upuuzi mtupu.
Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Quds amesema UNESCO iliwahi kuchukua maamuzi yanayouunga mkono utawala vamizi wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina na kwamba jumuiya hiyo ya kimataifa inapaswa kuchukua maamuzi yasiyopendelea upande wowote. Amezitaka pia nchi za Kiarabu na Kiislamu kususia shirika la UNESCO na kuacha kulitambua rasmi.
Maazimio ya Umoja wa Mataifa yanalitambua eneo la Quds Mashariki kuwa ni ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel.
826623