Mubarak al Badhali amepatikana na hatia ya kutusi Ushia na kutisha kumuua Saleh al Ashur mbunge Mshia katika Bunge la Kuwait.
Itakumbukwa kuwa mwaka 2010 al Badhali akiwa katika kituo cha polisi alimkosea heshima Saleh Ashur na kutusi madhehebu ya Kiislamu ya Shia. Sauti ya tukio hilo ilisambazwa katika intaneti. Mubarak al Badhuli ni mhubiri wa Kiwahabi kutoka Kuwait aliye na misimamo mikali ambaye analenga kuibua hitilafu za kimadhehebu baina ya Mashia na Masuni. 828105