Tawi hilo limefunguliwa katika sherehe iliyohudhuriwa na Balozi wa Iran nchini Indonesia Mahmoud Farazanzadeh na Mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran nchini humo Bw. Rabbani.
Tawi hilo limefunguliwa kufuatia mkataba kati ya Ikatan Jamaa Ahul Bait Indonesia (IJABI ) na taasisi 12 za harakati za vijana wa Kisuni katika mkoa huo.
Kwa mujibu wa Jalaluddin Rahmad mkuu wa IJABI, hii ni mara ya kwanza kwa tawi hilo kufunguliwa mkoani hapo. Amesema lengo kuu ni kustawisha ushirikiano wa Waislamu Mashia na Masuni.
Jumuiya ya Udugu wa Mashia na Masuni ilizunduliwa mjini Jakarta mwaka jana.
829268