Kwa mujibu wa gazeti la al Watan, kongamano hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Kiislamu na litafanyika Julai 28-29.
Fat'hi Abulward mkurugenzi wa idara ya kieneo ya jumuiya hiyo amesema itakuwa mara ya kwanza idara hiyo kuanda mkutano kama huo mjini Cairo.
Ameongeza kuwa Sheikh Mkuu wa Al Azhar Ahmad al Tayyeb pamoja na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Misri yatashiriki katika kongamano hilo.
"Kongamano hilo linalenga kuwasilisha taswira yenye mlingano kuhusu utambulisho wa mazungumzo ya Kiislamu katika dunia ya leo. Ni hatua ya kivitendo kuelekea katika ukuruba wa harakati za Kiislamu za Misri baada ya mapinduzi yaliyoanza Januari 25", amesema.
Fat'hi Abulward ameelezea matumaini kuwa washiriki watakuja na mapendekezo ambayo yatanusuru taifa la Misri kutokana na migogoro na hitilafu.
829396