Hujjatul Islam Hamid Mohammadi ambaye pia ni mkurugenzi wa maonyesho hayo amesema mjumuiko huo utahudhuriwa pia na Rais Mahmoud Ahmadinejad.
"Wanaharakati 3000 wa Qur'ani Tukufu watahudhuria mkutano huo ambapo Rais Ahmadinejad atawaenzi baadhi ya wanaharakati wa ngazi za juu wa Qur'ani nchini", amesema.
Ameongeza kuwa maonyesho ya mwaka huu yatakuwa na vitengo 30 ambavyo ni zaidi ya vya mwaka jana.
Hujjatul Islam Hamid Mohammadi amesema: "Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran ni tukio kubwa zaidi la Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu'. Ameendelea kusema kuwa maonyesho mengine 300 ya Qur'ani yatafanyika katika maeneo mengine ya Iran katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
829349