Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri imetoa taarifa ya dharura ikionya Shirika la Satalaiti la Nilesat kuwa iwapo kitarusha hewani filamu ya “ Al Hassan na Al Hussein” (AS) katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, basi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Kwa mujibu wa tovuti ya al Masrawi, kanali kadhaa za televisheni za satalaiti ambazo zinatumia satalaiti ya Nilesat zimesema zitarusha hewani filamu ya “Al Hassan na Al Hussein” AS katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo nyuso za Maimamu hao wawili zitaonyeshwa.
Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya Chuo Kikuu cha Al Azhar imeashiria fatuwa ya Al Azhar kuwa ni haramu kuonyesha nyuso za Ahul Bayt AS (Watu wa Nyumba ya Mtume SAW) na kusema filamu ya “Al Hassan na Al Hussein” AS haipaswi kurushwa hewani. 829883