Kwa mujibu wa tovuti ya Islamonline, Sheikhe Mkuu wa Al Azhar Ahmad Tayyib ameafiki uanzishwaji wa taasisi ya elimu Sudan Kusini kwa lengo la kufunza kwa kutumia mbinu ya Al Azhar na kutoa vyeti vyenye itibari kwa wanaohitimu.
Al Azhar imesema lengo la taasisi hiyo ni kueneza Uislamu wa misimamo ya wastani na kuipa nguvu lugha ya Kiarabu Sudan Kusini.
Imearifiwa kuwa Sheikh Ahmad Tayyib ametoa habari za kuasisi chuo hicho katika mkutano wake na Hassan Turabi kiongozi wa Chama cha Kongresi ya Taifa cha Sudan.
829930