Ofisi ya uongozi wa Masjidunnabi (saw) imetangaza kuwa msikiti huo uko tayari kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa watu wanaokwenda kuzuru kaburi la Mtume (saw) na kuwadhaminia utulivu kwa shabaha ya kusahilisha shughuli za kiibada.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma na Uenezi wa Msikiti wa Madina Abdul Wahid al Khattab amesema kuwa mipango ya msikiti huo katika mwezi wa Ramadhani imekwisha tayarishwa na kwamba maafisa wa msikiti wa Mtume wako tayari kutoa huduma bora kwa watu wanaokwenza kuzuru mtukufu huyo katika mwezi wa Ramadhani.
Ameongeza kuwa wafanyakazi wa Msikiti wa Mtume (saw) na wahudumu wake wako tayari kwa ajili ya msongamano mkubwa wa mazuwari wa msikiti huo katika mwezi wa Ramadhani na inakadiriwa kuwa watu milioni tatu watazuru kaburi la Mtume (saw) katika mwezi huo mtukufu. 829968