IQNA

Mkutano wa kimataifa wa Uchumi wa Kiislamu kufanyika Jiddah

16:16 - July 25, 2011
Habari ID: 2159786
Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi wa Kiislamu umepangwa kufanyika Jiddah, Saudi Arabia tarehe 10 na 11 Agosti.
Mkutano huo ambao umetayarishwa na kundi la al Barak la Bahrain utajadili masuala mbalimbali ya kiuchumi katika mtazamo wa Kiislamu.
Zaidi ya wafanyakazi 700 wa benki kuu za nchi za Kiislamu, wakuu wa mabenki, wakurugenzi wa taasisi za kifedha, maulamaa na wataalamu wa masuala ya uchumi wa Kiislamu watashiriki katika mkutano huo.
Vilevile nakala ya kwanza ya insaiklopedia ya Fiqhi ya Uchumi iliyotayarishwa na kundi la al Baraka itazinduliwa katika mkutano huo. 830627
captcha