IQNA

Tunisia Yatangaza Agosti Mosi kuwa Mosi Ramadhani

12:43 - July 26, 2011
Habari ID: 2160108
Tarehe Mosi Agosti imetangazwa kuwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Tunisia.
Tovuti ya Gnet imeripoti kuwa Kamati ya Istihlal (kuainisha mwezi mwandamo) imetoa taarifa na kusema kuwa, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, mwezi unaweza kuonekana tu Jumapili usiku, Julai 31.
"Kwa hivyo, Agosti mosi itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Rmadhani nchini Tunisia", imesema kamati hiyo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa kuna uwezekano mkondo huo ukafuatwa na nchi za Kiislamu kama Syria, Misri na Oman.
"Hata hivyo, katika baadhi ya nchi za Kiislamu kama Malaysia, Algeria, Indonesia, Morocco na nchi za Ghuba ya Uajemi, huenda mwezi mwandamo ukaonekana Jumamosi usiku na hivyo kuifanya Jumapili Julai 31 ikawa mwanzo wa Ramadhani katika nchi hizo", imesema taarifa hiyo.
830995
captcha