IQNA

Sheikh Mkuu wa Al Azhar apokea mwaliko wa kutembelea Iran

13:44 - July 27, 2011
Habari ID: 2160764
Nasser Sudani Mjumbe katika Majlisi (Bunge) ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amemkabidhi Sheikh Mkuu wa Al Azhar Ahmad Tayyib mwaliko rasmi kutoka kwa Spika wa Majilisi wa kutembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sudani alikabidhi mwaliko huo Jumanne 26 Julai wakati akiongoza ujumbe wa Kiirani uliokutana na Sheikh Ahmad Tayyib mjini Cairo.
Katika mkutano huo Sheikhe Mkuu wa Al Azhar amesisitiza umuhimu wa maelewano miongoni wa Waislamu na vilevile udharura wa kuwepo umoja kati ya Waislamu.
Sudani alikuwa Cairo kushiriki katika kongamano la Mapambano ya Kiislamu.
832480
captcha