IQNA

Viongozi wa dini za Mwenyezi Mungu kukutana Italia

16:59 - July 27, 2011
Habari ID: 2161102
Mkutano wa kimataifa wa viongozi wa dini za Uislamu, Ukristo na Uyahudi umepangwa kufanyika tarehe 27 Oktoba mwaka huu katika mji wa Assisi nchini Italia.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Nenedict XVI ametoa pendekezo la kufanyika mkutano huo wa viongozi wa dini za Mwenyezi Mungu kwa lengo la kufanya mazungumzo juu ya kuimarisha uhusiano kati ya dini mbalimbali sambamba na maadhimisho ya mwaka wa 25 tangu Papa John Puol wa II alipoitisha mkutano wa kwanza wa dini mbalimbali hapo tarehe 27 Oktoba mwaka 1986.
Mkutano huo wa kimataifa utahudhuriwa na viongozi wa makanisa, maulamaa wa Kiislamu na makuhani wa Kiyahudi.
Papa Benedict XVI ametangaza kuwa amani haiwezi kupatikana duniani isipokuwa kwa wanadamu kuchagua njia ya haki.
Imepangwa kuwa siku hiyo viongozi wa kila dini watafanya ibada za dini yao mbele ya wafuasi wa dini nyinginezo. 832689

captcha