Tovuti ya Toronto Muslims imeripoti kuwa mashindano hayo ambayo yatasimamiwa na Kituo cha Waislamu wa Toronto ni sehemu ya ratiba ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ya kituo hicho kwa ajili ya watoto.
Washiriki katika mashindano hayo watakuwa na wiki tatu za kwanza za mwezi wa Ramadhani kwa ajili ya kusoma maarifa ya Kiislamu na kisha kushiriki kwenye mashindano hayo.
Watoto wanaoshiriki katika mashindano hayo pia watatakiwa kuwa na daftari la kusajili matendo na amali zao nzuri katika kipindi chote cha mwezi wa Ramadhani kama vile kusoma na kuhifadhi Qur'ani, kusali, kuomba dua, kuwasaidia wenzao, kusoma vitabu na kadhalika.
Mwishoni mwa Ramadhani Kituo cha Waislamu cha Toronto kitatathmini kazi za wanafunzi hao na kuwapongeza kwa kuwapa zawadi mbalimbali. 832799