IQNA

Ufahamu wa Qur'ani, msingi wa Umoja wa Kiislamu

15:01 - July 30, 2011
Habari ID: 2162074
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu amesema msingi wa Umoja wa Kiislamu ni kufahamu kwa kina mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Akizungumza na IQNA, Ayatullah Muhammad Ali Taskhiri ameashiria nafasi ya harakati za Qur'ani katika kustawisha ukuruba wa Kiislamu na kusema: "Pamoja na Suna za Mtume SAW na kuwaapenda Ahul Bayt AS, tunapaswa kuongeza ufahamu wa mafundisho ya Qur'ani pamoja na hekima ya Qur'ani ili kuimarisha umoja wa Kiislamu.
Aidha ameashiria Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani yanayoendelea Tehran na kusema maonyesho kama hayo yanasaidia kuekelea kwenye umma moja.
833552
captcha