IQNA

‘Maadui wanavuruga amani eneo la Kurdistan’

15:05 - July 30, 2011
Habari ID: 2162077
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amesema maadui wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanazusha machafuko katika eneo la Kurdistan kaskazini magharibi mwa Iran ili kuzuia watu wa eneo hilo kupata huduma.
Akihutubia waumini katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Seddiqi amesema kundi la kigaidi la PJAK linatekeleza hujuma za kigaidi katika mipaka ya kaskazini maghairbi mwa Iran na eneo la Kurdistan nchini Iraq. Amepongeza hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, SEPAH, katika kupambana na kundi hilo la kigaidi.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran vile vile amelaani mauaji ya mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Khowjeh Nasrdin cha Tehran. Amesema mauaji hayo ya kigaidi yametekelezwa na majasusi wa utawala wa Kizayuni na kusema wanaounga mkono ugaidi wanazidi kuchukiwa duniani.
Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Seddiqi amesema mauaji ya wanasayansi wa Iran hayawezi kuzuia ustawi wa mfumo wa Kiislamu wa Iran. Amesema maadui wafahamu kuwa Jamhuri ya Kislamu ya Iran itaendelea na ustawi wa kisayansi na kila siku inatangaza mafanikio mapya duniani.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa pia ameashiria safari ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mkoa wa Hormozgan kusini mwa Iran. Amesema safari hiyo ya kukagua vikosi vya jeshi la wanamaji ilikuwa imejaa baraka. Amesema nguvu na uwezo wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kwa ajili ya kujihami na kudumisha amani na usalama katika eneo.
833407


captcha