Katika maandamano makubwa yaliyotajwa kuwa ya "Ijumaa ya Umoja " yaliyofanyika baada ya sala ya Ijumaa, waandamanaji wamesema wanataka mfumo wa Kiislamu. Maandamano yamefanyika kote nchini Misri ambapo mamilioni ya wananchi wamelitaka baraza la jeshi linalotawala nchi hiyo kukabidhi madaraka kwa wananchi na kusitisha kesi za raia katika mahakama za kijeshi.
Harakati ya Ikhawanul Muslimin na vyama vya upinzani ni miongoni mwa makundi yaliyoitisha maandamano hayo.
Haya yanajiri huku kesi dhidi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji na ufisadi ikitazamiwa kuanza kusikilizwa wiki ijayo.
Zaidi ya watu 800 waliuawa wakati wa harakati za mapinduzi zilizopelekea kung'olewa madarakani Mubarak mwanzoni mwa mwaka huu.
833834