IQNA

Qatar yawaalika wasomaji maarufu wa Qur'ani

16:32 - July 30, 2011
Habari ID: 2162085
Kwa mara ya kwanza Qatar imewaalika wasomaji 17 maarufu wa Qur'ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, imetangaza Idara ya Misikiti katika Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu nchini humo.
Maqarii hao wa Qur'ani ambao ni maarufu katika nchi za Kiarabu pia wataswalisha katika misikiti kadhaa ya Qatar.
Kati ya maqarii hao maarufu ni pamoja Dkt. Mohammed Abdul Karim, Idris Abkar, Abdel Wali Al Arkani, Abdul Mohsin Al Harthy, Abdul Majid Al Arkani, Yasin Fakieh, Muhammad Qassim, Marwan Al Herazy, Hamad Hassan, Mohammad Ahmad, Faris Abdullah, Mohammad Salem, Abdulrahim Al Qaabi, Mohamad Abdullah Hamza, Abdul Abdullah Hassan, Rashid Mohammad na Suleiman Mohammad Sheikh.
Mbali na kuswalisha pia watatoa darsa baada ya sala ambazo zitahusu fadhila za mwezi wa Ramadhani.
833425
captcha