"Alisikia abiria mwenzake akisoma Qur'ani na kuchukulia hatua hiyo kuwa tishio", amesema msemaji wa polisi Detlev Kaldinski mjini Rotenberg katika jimbo la Lower Saxony.
Wasiwasi wa mwanamke huyo ulipelekea dereva kusimamisha basi ambalo lilikuwa limebeba abiria 45 kutoka Copenhagen hadi Paris. Polisi walifika hapo wakiwa na kikosi maalumu na mbwa wa kusaka mabomu.
Upekuzi aliofanyiwa Muislamu huyo raia wa Tunisia ulibaini kuwa hakuwa na silaha wala mabomu. Mkasa huo ulipelekea barabara kufungwa kwa masaa mawili.
833789