Kitabu hicho ni katika silisila ya vitabu vya 'Kitab al Youm' vinavyotolewa kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mwandishi wa kitabu hicho anachunguza maisha ya makarii mashuhuri wa zama za dhahabu za kiraa ya Qur'ani nchini Misri kama Mohammed Siddiq Al-Minshawi na Abdul Basit Muhammad Abdul Samad ambao majina yao yamesajiliwa katika historia ya Misri.
Mwandishi wa kitabu hicho Nabiil Hanafi anasema kitabu chake kinachunguza na kuchambua historia ya Misri na serikali ya Kifatimi (Fatimid) ambayo ndiyo iliyoanzisha kwa mara ya kwanza maktaba za kufunza kiraa ya Qur'ani Tukufu katika miji na vijiji vya Misri.
Mhariri Mkuu wa silisila ya Kitabu al Youm, Nawal Mustafa anasema kuhusu kitabu cha Kitabu cha Nyota wa Zama za Dhahabu za Kiraa ya Qur'ani nchini Misri kwamba katika zama za sasa ambapo mafundisho ya kiraa ya Qur'ani hayafanyiki tena katika maktaba kama ilivyokuwa zamani, Redio Qur'ani ya Misri imetoa mchango mkubwa katika kuimarisha na kustawisha utamaduni wa Qur'ani. 833648