IQNA

Oxford kuandaa kongamano la kimataifa la ustaarabu wa Kiislamu

1:36 - August 03, 2011
Habari ID: 2164300
Taasisi ya Masomo ya Mashariki ya Kati na Afrika katika Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza inapanga kuandaa kongamano la kimataifa la ustaarabu wa Kiislamu.
Kongamano hilo limepangwa kufanyika Novemba mwaka huu ambapo mada zitakazojadiliwa ni pamoja na ufahamu wa ustaarabu, ufahamu wa ustaarabu wa Kiislamu, ufahamu wa ustaarabu, utamaduni na jamii. Aidha kongamano hilo litajadili mada kuhusu Qur’ani Tukufu, Sunna, muundo wa Uislamu, lugha ya Kiarabu, mfumo wa kifedha wa Kiislamu, elimu katika Uislamu n.k.
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha mukhtasari wa makala ni Septemba 20 na makala kamili zinapaswa kuwasilishwa kabla ya Oktoba 15.
Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo unaweza kutembelea tovuti ya http://www.oxfordimns.org.uk/
835641
captcha