Dk. Shein ameyasema hayo wakati akitoa risala ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa mwaka huu. Katika risala hiyo Dk. Shein, amesema Serikali kwa kupitia vyombo na taasisi zake imeandaa mazingira mazuri ya kufanyia biashara za vyakula katika mwezi wa Ramadhani na kusisitiza haja ya kufanyiana wema na hisani katika kipindi hicho chote.
Rais wa Zanzibar amekumbusha kuwa Saumu ina nguvu kubwa za kumuongoza mtu awe na tabia njema, subira, utulivu, upendo hata kwa wasio Waislamu.
Akinukuu aya ya 183 katika Suratul Baqara ndani ya Qur'an tukufu isemayo " Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu"
Dk. Shein ameongeza kuwa "Haya ni mambo ambayo tunapaswa kuyatafuta kwa nguvu na imani zetu ili tufanikishe Saumu yetu, misingi mikubwa ya mambo hayo ni imani na ihsani, tukiwa na ihsani tutakuwa waumini na ndivyo tulivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu,"
836706