IQNA

Wiki ya Qur’ani Tanzania katika Mwezi wa Ramadhani

15:29 - August 04, 2011
Habari ID: 2165058
Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Tanzania amesema ‘Wiki ya Qur’ani imeandaliwa nchini humo katika wiki ya tatu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mortadha Saburi amesema programu za wiki hiyo zitajumuisha mashindano ya Qur’ani katika vitengo vya hifdhi na qiraa.
Aidha kutakuwepo vikao vya Qur’ani vitakavyohudhuriwa na maqarii kutoka Iran.
Saburi ameongeza kuwa baadhi ya programu hizo zitafanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Iran na vilevile katika baadhi ya misikiti kama Msikiti wa Al Ghadir mjini Dar es Salaam.
Ameendelea kusema kuwa kutakuwepo mashindano ya Qur’ani katika Idhaa za Radio Kheir na Radio Qur’an na hafla za Iftar. Aidha amesema magazeti ya Tanzania yatachapisha hotuba za Imam Khomeini RA na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu Qur’ani Tukufu na mwezi mtukufu wa Ramadhani.
836119
captcha