IQNA

CD ya programu za Qur’ani ya Ridhwan-2 katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tehran

15:48 - August 09, 2011
Habari ID: 2167963
CD yenye programu za Qur’ani ya Ridhwan-2 inauzwa katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani yanayoendelea mjini Tehran.
CD hiyo ya Ridhwan-2 inakusanya majmui ya maarifa ya Kiislamu na sayansi ya Qur’ani.
Miongoni mwa programu za CD hiyo ni pamoja na tarjumi ya sauti ya Qur’ani Tukufu kwa sauti ya Samawati, makharijil huruf, mahadhi ya kiraa, tajwidi ya Qur’ani, kamusi ya maudhui na kamusi ya misamiati ya Qur’ani, faharasi ya maneno ya Qur’ani, mafunzo ya hifdhi ya Qur’ani katika awamu tano, kiraa za wasomaji mashuhui wa Qur’ani wa kimataifa, matini kamili ya Nahjul Balagha, kisomo na tarjumi yake kwa lugha za Kiingereza na Kifarsi, matini kamili ya Sahifa Sajjadiyya, kisomo na tarjumi yake kwa lugha za Kiingereza na Kifarsi.
CD hiyo pia ina kiraa ya tajwidi ya Minshawi, Ustadh Parhizgar na tafsiri za Qur’ani za al Mizan kwa lugha za Kiarabu na kifarsi, tafsiri za al Amthal, Majmaul Bayan, Rahnamaa, Nur, Tasnim na Kauthar na tarjumi ya Qur’ani kwa lugha saba hai duniani.
CD hiyo pia ina kitabu cha dua cha Mafatihul Jinan, hadithi za Maasumin, maktaba ya vitabu vya Kiislamu, visa vya Mitume na kadhalika. 840033
captcha