Duru za kidiplomasia zinasema Uturuki imetoa wito kwa OIC kuitisha kikao hicho maalumu ili kujadili hali ya njaa na ukame barani Afrika na hasa nchini Somalia.
Mapema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Ahmet Davutoglu alikutana na Katibu Mkuu wa OIC Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu ambapo walijadilia suala la misaada ya dharura kwa wanaokumbwa na njaa nchini Somalia.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia imetoa ombi la mkutano wa dharura wa OIC kujadili njia za kuwanusuru wanaokumbwa na njaa barani Afrika.
840629