Kozi hiyo ni ya tano tokea ianzishwe na kufadhiliwa na Waqfu wa Sheikh Eid Bin Muhammad al Thani wenye makao yake Qatar. Waqfu huu unatoa misaada katika nchi 18 kote duniani kupitia taasisi 32 za Kiislamu zinazotoa himaya kwa mayatima 7000 duniani.
Lengo la kozi hiyo limetajwa kuwa ni kutoa mafunzo ya kuwafanya mayatima hao wawe raia wema wanaojitegemea.
Naibu Mkuu wa Idara ya Jamii nchini Gambia Fallu Sowe amesema serikali ya nchi hiyo inalipa umuhimu mkubwa suala la elimu na maisha bora ya watoto hasa mayatima.Ameishukuru taasisi ya Ummul Quraa kwa misaada yake. Aidha aimetoa shukrani kwa familia ya Mfalme wa Qatar ambayo imefadhili kozi hiyo. 840510