IQNA

Kazi bora za sanaa ya Qur’ani katika maonyesho ya Qur’ani Tehran

13:33 - August 10, 2011
Habari ID: 2168349
Mkuu wa Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran amesema kazi bora na teule za sanaa ya Qur’ani zitazinduliwa wiki ya tatu ya maonyesho hayo.
Hujjatul Islam Hamid Mohammadi amesema kuwa katika wiki ya kwanza kazi bora zilizochapishwa zilionyeshwa na pia Tarjumi ya Qur’ani Tukufu kwa Kifarsi ya Gholam Ali Haddad Adel ilizinduliwa.
Mohammadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu anayesimamia masuala ya Qur’ani amesema kuwa katika maonyesho ya mwaka huu kuna kitengo maalumu cha familia pamoja na programu kuhusu mwamko wa Kiislamu na Hijabu.
Amesisitiza kuwa mwaka huu suala la mwamko wa Kiislamu limepewa umuhimu katika maonyesho hayo.
840393
captcha