Hujjatul Islam Hamid Mohammadi amesema kuwa katika wiki ya kwanza kazi bora zilizochapishwa zilionyeshwa na pia Tarjumi ya Qur’ani Tukufu kwa Kifarsi ya Gholam Ali Haddad Adel ilizinduliwa.
Mohammadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu anayesimamia masuala ya Qur’ani amesema kuwa katika maonyesho ya mwaka huu kuna kitengo maalumu cha familia pamoja na programu kuhusu mwamko wa Kiislamu na Hijabu.
Amesisitiza kuwa mwaka huu suala la mwamko wa Kiislamu limepewa umuhimu katika maonyesho hayo.
840393